KINSHASA: Matokeo ya uchaguzi yangojewa Kongo
13 Agosti 2006Matangazo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,kura za kumchagua rais,zilizopigwa Julai 30 zinaendelea kuhesabiwa.Baada ya takriban asilimia 20 ya kura kuhesabiwa,rais wa hivi sasa Joseph Kabila anaongoza kwa asilimia 53.Mhasimu wake mkuu,naibu rais na aliekuwa kiongozi wa waasi,Jean-Pierre Bemba amepata kama asilimia 17 ya kura.Wagombea urais 19 kutoka jumla ya 33 wameungana kulalamika kuwa uchaguzi umefanyiwa udanganyifu.Matokeo ya mwisho yanatazamiwa kutangazwa tarehe 20 Agosti.
