1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa: Mtoto wa Mobutu arudi nyumbani

24 Novemba 2003

Mtoto wa kwanza wa kiume wa aliyekuwa dikteta wa Zaire, Mobutu Sese Seko amerudi nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa muda wa miaka sita. Manda Mobutu, alipowasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kinshasa akitokea Paris, Ufaransa amelakiwa na mdogo wake wa kiume na ujumbe maalumu wakiwemo waliokuwa Walinzi wa Baba yake. Manda Mobutu, aliyekuwa uhamishoni Moroko, Ivory Coast na Ufaransa hakusema chochote alipowasili. Hata hivyo, hivi karibuni amesema kuwa ana adhma ya kufukua maiti ya Baba yake nchini Moroko ili ikazikwe tena Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Mobutu, aliyeitawala nchi hiyo kwa muda wa miaka 32 na kuiacha utupu licha ya utajiri wake mkubwa, amefariki uhamishoni nchini Moroko mwaka 1997, muda mfupi baada ya kupinduliwa na aliyekuwa Kiongozi wa waasi, Laurent Kabila, Baba wa Rais wa wakati huu Joseph Kabila.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW