KINSHASA: Ndege ya abiria yatoweka Kongo
26 Mei 2005Matangazo
Ndege iliyokuwa na abiria 19 na wafanyikazi watano imetoweka huko mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa zaidi ya saa kumi.
Kwa mujibu wa mkuu wa safari za ndege nchini humo ndege hiyo aina ya Antonv 12 iliondoka kutoka Goma saa nyingi na ilitarajiwa kurudi Kindu lakini mawasiliano waliyoyapata ni kwamba ndege hiyo haikuwasili Kindu.
Ndege nyingine zilipelekwa kuitafuta ndege hiyo iliyotoweka ikiwa ni pamoja na Helikopta za Umoja wa Mataifa lakini hakuna kilichoonekana.
Watu kumi waliuwawa mapema mwezi huu baada ya ndege aina hiyo kuanguka kwenye miti na kuwaka moto katika eneo la Kaskazini mashariki mwa Kongo katika mji wa Kisangani.