KINSHASA: Uchaguzi umeahirishwa nchini Congo
18 Juni 2005Matangazo
Bunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limepiga kura kurefusha hadi Desemba mwaka huu kipindi cha mpito cha kisiasa.Muda wa kipindi hicho ulikuwa ukimalizika mwisho wa mwezi huu.Mkuu wa kamisheni ya uchaguzi amesema muda huo umehitaji kurefushwa kwa miezi sita mingine ili kuweza kufanya matayarisho ya uchaguzi.Takriban wabunge 500 wamepiga kura kuunga mkono kurefisha kipindi hicho cha mpito.Wengine 14 walipinga pendekezo hilo.Msingi wa makubaliano yaliopatikana mwaka 2003 ni kuwa na uchaguzi huru wa mwanzo nchini humo tangu miaka 40 ya nyuma.Makubaliano ya mwaka 2003 yamemaliza vita vya miaka mitano nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.