1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Umoja wa Mataifa waunga mkono hatua ya walinda usalama nchini Kongo

3 Machi 2005

Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wamewauwa takriban wanamgambo 50 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema makabiliano na wanamgabo hao yalianza baada ufyatulianaji risasi na walinda usalama kutoka Pakistani.

Makabiliano hayo yalifanyika takriban kilomita 30 nje ya mji wa Bunia mji mkuu wa eneo la mzozo la Ituri. Mjini New York baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeunga mkono hatua ya walinda usalama huku likilaani mauaji dhidi ya walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh.

Kiongozi wa kundi hilo la wanamgambo alikamatwa mapema mjini Kinshasa kuhusiana na uvamizi uliofanyika wiki iliyopita ambapo walinda usalama 9 kutoka Bangladesh waliuwawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW