1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Wanajeshi wa kimataifa wapiga doria

24 Agosti 2006
Waziri mkuu wa hungary ajiuzulu-dai la wapinzani.
Waziri mkuu wa hungary ajiuzulu-dai la wapinzani.Picha: AP

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na wale wa Umoja wa Ulaya wamekuwa wakipiga doria katika mitaa ya Kinshasa kurudisha utulivu katika mji huo mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Inaonekana kwamba usitishaji wa mapigano kati ya makundi hasimu ya kisiasa unafanya kazi.Maduka yamefunguliwa tena na waakazi wametoka nje mitaani kwa mara ya kwanza tokea kuzuka kwa mapigano makali hapo Jumapili kati ya walinzi wa Rais Joseph Kabila na askari tiifu kwa mpinzani wake wa kisiasa Jean- Piere Bemba.

Mapigano hayo yalizuka Jumapili baada ya kutangazwa kwamba wagombea hao wawili wa Urais watarudiana katika duru ya pili ya uchaguzi mwezi wa Oktoba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW