1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Wanamgambo 18 wauwawa

3 Aprili 2005

Takriban wanamgambo 18 wameuwawa baada ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kupambana na wanamgambo wenye silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa amesema mapigano hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya operesheni ya kijeshi ya kuwapokonya silaha waasi baada ya muda wa mwisho wa kusalimisha silaha hizo kwa hiari kumalizika. Msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini CONGO MONUC amesema walinda amani hao walifyatuwa risasi baada tu ya kushambuliwa na wanamgambo hao.Wanajeshi wa Bangalesh na Pakistan walihusika katika operesheni hiyo.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya wanamgambo 8,000 kati ya wanaokadiriwa kufikia 15,000 katika jimbo la Ituri wamesalimisha silaha zao kufikia tarehe Mosi Aprili ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho iliowekwa kusalimisha silaha hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW