KINSHASA: Wananchi wapiga kura nchini Kongo
30 Julai 2006Matangazo
Uchaguzi mkuu wa kwanza ulio huru tangu miaka 46 ya nyuma,unafanywa hii leo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wadhifa wa rais unagombewa na watetezi 32 na zaidi ya wagombea 10,000 wanataka kuingia katika bunge lenye viti 500.Rais wa hivi sasa,Joseph Kabila katika hotuba yake kwenye televisheni alitoa mwito kwa wananchi kwenda kupiga kura.Kikosi cha kimataifa cha wanajeshi 19,000 kipo nchini Kongo kusaidia kulinda usalama wakati wa uchaguzi.Miongoni mwa wanajeshi hao,800 ni kutoka Ujerumani.
