1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wasiwasi wa kuzuka magonjwa nchini Kongo

7 Machi 2005

Hatari ya kuzuka kwa magonjwa imeongezeka kwa kiwango cha kutisha Kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema zaidi ya wakimbizi elfu 70 wamekimbilia kwenye kambi za wakimbizi ambapo tayari kunamsongamano wa watu baada ya kuzuka upya kwa mapigano kwenye eneo la Ituri.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na yasiyo ya kiserikali ya kutoa msaada yamesimamisha shughuli za kutoa msaada katika eneo hilo la mzozo. Hatua hiyo huenda ikasababisha zaidi ya wakimbizi wapatao elfu 54 kukosa chakula na huduma za matibabu kwa muda wa wiki moja.

Hatua hiyo imetokana na mashambulizi ya hivi karibuni ambapo zaidi ya wanamgambo 50 waliuwawa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW