KINSHASA
16 Februari 2005Matangazo
Wanafunzi tisa wa shule wameuawa kwa kupondwa na mawe baada ya lori lililokuwa limejaza mawe kuwaangukia katika mji wa kusini wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Wanafunzi hao walikuwa ndio kwanza wanatoka shuleni na walikuwa wanasubiri kuvuka barabara ndipo walipoangukiwa na mawe yaliyokuwa yamejazwa katika lori moja,baada ya dereva wake kushindwa kulimudu.
Ajali hiyo imetokea kilometa 20 kutoka mji wa Lubumbashi mji mkuu wa jimbo la kusini-mashariki la Katanga.