1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Umoja wa Mataifa waombwa kutoondoa askari wake DRC

10 Januari 2007

Taasisi kubwa isiyo ya kiserikali yenye makao yake Brussels Ubelgiji, imeitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza zaidi misaada kwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taasisi hiyo imesema kuwa ni kwa njia hiyo tu ndiyo amani iliyoanza kurejea nchini humo, itaweza kudumu.

Katika taarifa yake, iliyotolewa mjini Brussels jana, taasisi hiyo imesema kuwa askari elfu 17 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wanatakiwa kubakia huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo angalau mpaka mwisho wa mwaka huu.

Nchi hiyo ya Afrika ya Kati mwishoni mwa jana ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia toka ipate uhuru miaka 40 iliyopita ambapo Rais Joseph Kabila alichaguliwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW