KINSHASA:Visa 9 vya Ebola vyathibitishwa Kasai Magharibi
22 Septemba 2007Visa tisa vya ugonjwa wa Ebola vinathibitishwa kutokea katika eneo la Kasai magharibi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Mlipuko huo wa Ebola unaripotiwa kusababisha vifo vya yapata watu 174 kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO.
Ugonjwa huo ulio na ishara za viwango vya juu vya joto la mwili,kuendesha na kutokwa damu uliogunduliwa kwanza mwishoni mwa mwezi Aprili katika eneo la Kampungu lililo magharibi mwa Kasai.Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF tawi la Belgium linasema kuwa watu 5 wana virusi hivyo katika kliniki yao ya Kampungu.
Visa 400 vimeripotiwa kutokea nchini humo vikiwemo Shigella ambao ni ugonjwa wa kuendesha damu.Hakuna tiba yoyote ya ugonjwa wa Ebola kwa sasa unaosababisha kuvuja kwa damu kwenye viungo vya ndani.