1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Waasi wa Laurent Nkunda wajisalimisha kwa Umoja wa mataifa

19 Machi 2007

Raia 10 wa Rwanda wanaodai kusajiliwa bila kujua na kundi la waasi walio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamejisalimisha kwa kikosi cha Umoja wa mataifa.

Kulingana na msemaji wa kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa Sylvie van den Wildenburg,watu hao walidanganywa na Jenerali Laurent Nkunda kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini kwa madai ya kupewa nafasi za kazi. Umoja wa mataifa kwa upnade wake unaendelea na mpango wa kuwarejesha nchini Rwanda.Serikali ya Kinshasa imeanzisha mpango wa kujaribu kutafuta suluhu ya ghasia katika eneo hilo la Kivu ya Kaskazini kwa kuunda vikosi vinavyoshirikisha majeshi ya serikali na wafuasi wa Laurent Nkunda.

Kundi la Waasi la Maimai vilevile Wanyarwanda wanaopinga serikali ya Kinshasa bado wanaendesha shughuli zao katika eneo hilo.Hata hivyo unyanyasaji katika wakazi wa eneo hilo bado unaendelea na zaidi ya watu alfu 50 waliyakimbia makazi yao mwezi wa Februari.Kulingana na maafisa wa serikali maelfu ya raia wa Rwanda wamehusishwa katika mpango huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW