KINSHASA:Wanajeshi wa Kongo na Uganda kushirikiana
8 Agosti 2007Matangazo
Maafisa wa kijeshi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na wenzao wa Uganda wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kulainisha hasli tete iliyozuka katika eneo la mpaka la mto Albert baada ya machafuko ya siku chache zilizopita yaliyosababisha kuuwawa watu wawili.