1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´ chawadia Marekani

5 Machi 2024

Majimbo zaidi ya 15 ya Marekani yanapiga kura za mchujo leo kuamua wagombea wa urais wa vyama vikuu viwili vya Democratic na Republican kuelekea uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Marekani| Michigan
Bango la kuonesha eneo la kupiga kura ya mchujo Marekani Picha: Paul Sancya/AP/picture alliance

Rais Joe Biden anayewania muhula wa pili bila upinzani mkubwa kupitia chama cha Democratic anatazamiwa kupata ushindi wa wazi kwenye kura hizo zinazofanyika katika majimbo 16 na eneo jingine moja lililo chini ya milki ya Marekani.

Kwa upande wa Rebuplican, uchaguzi huo wa mchujo unaofahamika pia kama "kinyang´anyiro cha Jumanne Kuu" unatazimiwa kufungua milango zaidi kwa rais wa zamani Donald Trump kuelekea kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa mwezi Novemba.

Tangu kuanza kwa kura za mchujo Trump ameshinda kwenye majimbo yaliyokwishapiga kura huku mpinzani wake aliyebakia Nikki Haley alipata ushindi wa kwanza hapo jana kwenye wilaya ya Washington DC.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW