Kinyang'anyiro cha Ligi ya Premier chapamba moto
3 Aprili 2017Wakiwa pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, nambari mbili Spurs na pengo la pointi saba kati yao, wanasafiri kucheza dhidi ya Swansea wanaopambana kuepuka kushushwa daraja wakati Chelsea wataantgushana na Manchester City wakilenga kuepuka kichapo cha pili mfululizo.
Wiki moja iliyopita, kinyang'anyiro cha ubongwa kilionekana kuwa kimekishwa kabisa lakini sasa kitarejea tena kama Chelsea, waliozabwa na Crystal Palace nyumbani mwishoni mwa wiki, watazabwa tena nyumbani dhidi ya Manchester City Jumatano wiki hii.
Nambari tatu Liverpool huenda watakosa huduma za Sadio Mane ambaye ni majeruhi, wakati watakutana na Bournemouth. Liverpool waliwazaba Everton 3-1 na wana pointi moja juu ya Man City ambapo walitoka sare ya 2-2 na Arsenal ijapokuwa wamecheza mechi moja zaidi.
Manchester United ambao walitoka sare ya 0-0 nma West brom watasuka dimbani dhidi ya Everton kesho Jumanne, na kama mambo yalivyo, itakuwa vigumu kumaliza katika nne bora. Arsenal watakwaruzana na West Ham United.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga