1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

kinyang'anyiro cha urais chaendelea kushika kasi Marekani

24 Julai 2024

Baada ya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais, Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuhutubia taifa.

Marekani | Rais Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden atarajiwa akitoa hotuba.Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Makamu wake Kamala Harris akitarajia kuelekea katika jimbo la Indiana, na Donald Trump kufanya kampeni yake ya kwanza tangu Biden alipojiondoa kwenye kinyanganyiro cha urais. 

Itakuwa siku ya pilka pilka nyingi nchini Marekani wakati kampeni zikiendelea kupamba moto.

Hotuba ya Biden usiku wa leo inatarajiwa kutoa taswira ya urathi anaouacha katika siasa za Marekani na kwa Harris kuendelea kutetea sifa wa mtangulizi wake kwa kuzingatia upya sheria za ndani, ushirikiano wa nje, na ulinzi wa demokrasia.

Soma pia: Scholz asema Harris huenda akashinda uchaguzi wa Marekani

Ingawa Biden hatoshiriki kwenye kura ya Novemba, wapiga kura bado wanataka kupima uthabiti wa urathi wake. Harris anachukua nafasi yake kama mshika bendera wa chama cha Democrats, katika wakati mafanikio ya Biden yako hatarini iwapo Mrepublican Donald Trump atashinda uchaguzi huo.

Viongozi wa Republican wanawaonya wanachama wake dhidi ya kutumia kwa uwazi matamshi ya kibaguzi na kijinsia dhidi ya Makamu wa Rais Kamala Harris, wakati wakitafakari jinsi gani ya kupamabana na mpinzani huyo wa Trump chini ya miezi minne kabla Siku ya Uchaguzi.

Katika mkutano wa faragha wa wabunge wa Republican, Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kamati ya Wabunge wa Republican Richard Hudson, amewataka wabunge hao kushikamana na kumkosoa Harris kwa kuhoji jukumu lake katika sera za utawala wa Biden.

Donald Trump anafanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara wa kampeni tangu Rais Joe Biden alipojiondoa kwenye kinyanganyiro cha urais na kumwacha rais huyo wa zamani kuelekeza hasira zake kwa mpinzani wake mpya.

Shinikizo kwa Netanyahu

Rais Joe Biden akutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas.Picha: Evelyn Hockstein/File Photo/REUTERS

Haya yanajiri huku kukishuhudiwa maandamano yaliopangwa katika majengo ya bunge na baadhi ya waandamanaji wakilaani kampeni ya kijeshi ya Israeli kwa ujumla, na wengine wakionyesha kuiunga mkono Israel, lakini wakimshinikiza Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kukubali mpango wa kusitisha mapigano ili kuwarudisha nyumbani mateka.

Soma pia: Kamala Harris aungwa mkono kugombea urais Marekani

Netanyahu anatarajia kulihutubia bunge la Marekani kuhusu msingi wa vita vinavyoendelea huko Gaza. Hata hivyo baadhi ya wanachama wa Democrats wamesusia kuhudhuria mkutano waziri mkuu huyo. Seneta wa Maryland Chris Van Hollen, anaeleza kwanini hatohuduria mkutano huo.

"Rais Biden ametoa kipaumbele kwa kurudi salama kwa mateka wote. Waziri Mkuu Netanyahu hajafanya hivyo. Anaendelea kutanguliza maslahi yake ya kisiasa badala ya maslahi ya watu wa Israel na raia wa Marekani. Kwa hiyo namwambia Netanyahu kabla ya kuja kulihutubia bunge nenda kwanza ukakutane na familia za waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulio la Oktoba saba ."

Baada ya hotuba kwa bunge, Netanyahu pia anatarajiwa kukutana na Trump katika jimbo la Florida siku ya Ijumaa licha ya kuwa na uhisiano mdogo wakati wa utawala wake.

Trump akubali kuwa mgombea wa Republican 2024

02:32

This browser does not support the video element.