Bazoum ataka mahakama ya kikanda itoe amri ya kuachiwa kwake
21 Septemba 2023Matangazo
Kwenye maombi yaliyowasilishwa mahakamani wiki hii, Bazoum anataka Jumuiya hiyo ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS itangaze kuwa uamuzi wa wanajeshi kumweka kizuizini, unakiuka haki zake za msingi na kwamba yeye bado ni kiongozi halali wa Niger.
Bazoum aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya Julai 26 na tangu wakati huo, yeye pamoja na familia yake wanashikiliwa na wanajeshi waliochukua madaraka.
Macron asema balozi wake nchini Niger anaishi kama mateka
LichNiger yaituhumu Ufaransa kutaka kuishambuliaa ya shinikizo la kimataifa, majenerali waliompindua wamekataa miito ya kumwachia huru au kumrejesha madarakani na wao kuachia hatamu za kuliongoza taifa hilo.