1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi aliyetoweka wa waasi Nigeria atangaza yuko Israel

Caro Robi
22 Oktoba 2018

Kiongozi aliyetoweka wa waasi nchini Nigeria Nnamdi Kanu anayetaka kuundwa taifa lao la Biafra, atangaza yuko Israel.

Nigeria Biafra | Nnamdi Kanu
Picha: DW/K. Gänsler

Kiongozi aliyetoweka wa waasi wanaotaka kujitenga nchini Nigeria wakipigania kuundwa taifa lao la Biafra, ametoa tangazo kwa njia ya Redio akisema yuko nchini Israel, na kwamba dola ya Kiyahudi inajukumu la kulinda maisha yake.

Kiongozi huyo wa chama cha watu asili wa Biafra- IPOB, Nnamdi Kanu na ambaye alizungumza kupitia kituo cha redio kilichoko mafichoni kinachojiita Radio Biafra hakuonekana hadharani tangu Septemba mwaka jana.

Kanu anashikilia kwamba watu wa kabila la Igbo ambao ndio wengi kusini mashariki mwa Nigeria ni kabila la Israel lililopotea na ni jukumu kuliongoza taifa la Biafra alililoliita takatifu.

Kumekuweko na uvumi kwamba Kanu yuko nchini Israel baada ya kuonekana katika mkanda wa video akiwa kwenye ukuta wa magharibi wa Jerusalem, na kuzusha maswali vipi alifanikiwa kuondoka Nigeria.

Kanu anakabiliwa na mashitaka ya uhaini nchini Nigeria na alikuwa ameachiwa kwa dhamana, na wanajeshi kuwekwa nje ya nyumba yake mjini umwahia katika jimbo la kusini mashariki la Abia Septemba 2017.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW