1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Puigdemont wa Catalonia aukodolea macho uchaguzi ujao

21 Machi 2024

Aliyekuwa kiongozi wa jimbo la Catalonia linalotaka kujitenga Carles Puigdemont hii leo anatarajiwa kuzindua mipango yake kwa ajili ya uchaguzi wa mapema kwenye jimbo hilo.

Uhispania l Carles Puigdemont
Kiongozi anayetaka kujitenga kwa jimbo la Catalonia la Uhispania Carles PuigdemontPicha: Dwi Anoraganingrum/Geisler-Fotopress/picture alliance

Hatua hiyo inaashiria huenda sasa akarejea nyumbani baada ya miaka kadhaa ya kuishi uhamishoni.

Mbunge huyo wa Ulaya aliyekimbilia Ubelgiji kuepuka kushitakiwa dhidi ya jaribio lililoshindwa la kujitenga mnamo mwaka 2017 anatarajiwa kutangaza ikiwa atagombea kwenye uchaguzi huo wa mwezi Mei.

Ameandika kwenye mtandao wa X kwamba watarejea nyumbani kwa sababu ileile iliyowafanya kukimbilia uhamishoni kwa ajili ya mustakabali wa taifa lao.

Wiki iliyopita, kiongozi wa sasa wa Catalonia Pere Aragones aliitisha uchaguzi wa mapema kwenye jimbo hilo tajiri la kaskazini mashariki mwa Barcelona, katika mkesha wa kura muhimu ya bunge la Uhispania lililoidhinisha sheria ya msamaha kwa wanaotaka kujitenga wa Catalonia.