1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Kiongozi mpya wa Syria asema serikali itadhibiti silaha zote

Saleh Mwanamilongo
23 Desemba 2024

Hatua hiyo inafuatia wasiwasi wa nchi jirani na zile za magharibi juu ya uwezekano wa kuenea kwa silaha nchini Syria baada ya kuanguka kwa utalawa wa Bashar Al Assad.

Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al Sharaa (Kulia ) na waziri wa mamabo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan, mjini Damascus 22.12.2024
Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al Sharaa (Kulia ) na waziri wa mamabo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan, mjini Damascus 22.12.2024 Picha: Turkish Foreign Ministry/DIA Images/ABACA/picture alliance

Kiongozi mpya wa Syria , Ahmed al Sharaa amesema vikundi vilivyojihami vya Syria vitaanza kutangaza kuvunjwa kwao na kuingia jeshini. Ameyasema hayo kufuatia mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan.

Awali, kiongozi huyo mpya wa Syria alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Lebanon na kuapa kukomesha "uingiliaji hasi" wa Syria katika nchi hiyo jirani.

"Tulikuwa na mazungumzo marefu na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki juu ya hali na changamoto za siku zijazo nchini Syria ikiwa ni pamoja na changamoto za usalama, uchumi na aina ya muundo wa kisiasa wa baadaye wa Syria.", alisema Sharaa.

Alienbdelea kusema : "Pia, ungaaji mkono kutoka nchi jirani. Pia, tulijadili suala la kuunga mkono na kuimarisha serikali ijayo na hasa wizara ya ulinzi ambapo silaha zitakuwa mikononi mwa dola pekee na silaha zisiwe nje ya udhibiti wa dola."

Waasi wanaoungwa mkono na Uturuki waliliunga mkono kundi la Kiislamu la Sharaa Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambalo liliongoza muungano wa waasi ulioangusha wa Bashar al-Assad wiki mbili zilizopita.

"Syria kwa Wasyria wote"

Iran imesema haina mawasiliano yoyote hadi sasa na utawala mpya wa DamascusPicha: BAKR ALKASEM/AFP/Getty Images

Jumapili , kiongozi mpya ya Syria alionekana akivaa suti na tai wakati wa mikutano yake katika ikulu ya rais, kinyume na siku za nyuma ambapo alikuwa akivaa shati la kijeshi la kijani kibichi. Katika tangazo jingine, Ahmed al-Sharaa amesema watashughulikia kulinda madhehebu ya walio wachache dhidi ya mashambulizi yoyote. Huku akiongeza kuwa Syria ni nchi ya Wasyria wote na wanaweza kuishi pamoja.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Hakan Fidan amesema vikwazo dhidi ya Syria lazima "viondolewe haraka iwezekanavyo". Fidan alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhamasishwa kusaidia Syria kurejea kwenye uongozi bora na watu waliokimbia makazi yao kurejea.

Viongozi wa kimataifa wamiminika Damascus

Toka kuanguka kwa utawala wa Bashar Al Assad, viongozi kadhaa wa nchi za kikanda na kimataifa wametembelea Syria kukutana na viongozi wapya nchini humo.

Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi amekutana na kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa mjini Damascus ikiwa ni ziara ya kwanza ya ngazi ya juu ya nchi hiyo tangu kuondolewa kwa Bashar al-Assad.

Kwa upande wake Iran imesema inaunga mkono mamlaka ya Syria na kusema nchi hiyo haipaswi kuwa kimbilio la ugaidi baada ya kuanguka kwa rais Bashar al-Assad. Hata hivyo utawala wa Tehran umesema haujakuwa na mawasiliano yoyote na utawala mpya wa Damascus.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW