1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Belarus asema Putin amejitolea kusaidia

16 Agosti 2020

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema rais wa Urusi Vladimir Putin amejitolea kuhakikisha usalama nchini humo huku waandamanaji wa upinzani wakiongeza shinikizo dhidi ya kiongozi huyo mkongwe

Belarus Minsk Lukaschenko Ministersitzung
Picha: Reuters/M. Guchek

Mamia ya waandamanaji wa upinzani walikusanyika katika mji mkuu Minsk katika eneo ambalo mwandamanaji mmoja alifariki wakati wa ukandamizaji wa polisi wiki iliyopita dhidi ya maandamano ya kupinga madai hayo ya Lukashenko kwamba aliibuka mshindi katika uchaguzi huo wa Jumapili.

Akikabiliwa na changamoto kubwa zaidi katika uongozi wake tangu kuchukuwa hatamu za uongozi mwaka 1994, Lukashenko ameomba usaidizi wa Urusi na kuzungumza na Putin kwa njia ya simu baada ya kuonya kuwa kuna tishio sio tu kwa Belarus.

Waandamanaji waliokamatwa walielezea kuteswaPicha: picture-alliance/dpa/N. Fedosenko

Baadaye aliwaambia wakuu wa jeshi kuwa Putin alitoa msaada mpana wa kuhakikisha usalama wa Belarus.

Ikulu ya Urusi imesema viongozi hao walikubaliana "matatizo" nchini Belarus "yatatatuliwa hivi karibuni" na mahusiano ya nchi hizo kuimarishwa.

Katika mkutano na wakuu wa jeshi, Lukashenko alifuta uwezekano wa upatanishi wa kigeni kati yake na waandamanaji. "Hatutaisalimisha nchi kwa yeyote," alisema katika kauli zilizorushwa kwenye televisheni. "Hatuhitaji serikali zozote za kigeni, wapatanishi wowote."

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo Jumamosi alimhimiza Lukashenko "kushirikiana na makundi ya kiraia" wakati akiwa ziarani Poland, ambayo imejitolea kutumika kama mpatanishi.

Upinzani unapanga maandamano makubwa Jumapili ambapo watafanya "Matembezi ya Uhuru" katika barabara za katikati ya mji mkuu Minsk.

afp

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW