1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa genge la uhalifu Messina Denaro yuko mahututi

23 Septemba 2023

Kiongozi wa kundi la Mafia wa Italia, Matteo Messina Denaro, ambaye alitiwa mbaroni Januari baada ya kuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 30, yupo mahututi akiwa amepoteza fahamu

Italienischer Mafiaboss im Koma
Picha: ITALIAN CARABINIERI PRESS OFFICE/AFP

Kiongozi wa kundi la Mafia wa Italia, Matteo Messina Denaro, ambaye alitiwa mbaroni Januari baada ya kuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 30, yupo mahututi akiwa amepoteza fahamu tangu Ijumaa.Madaktari katika kituo anachopatiwa matibabu mjini L'Aguila wametangaza kuwa Denaro anaugua saratani ya utumbo na kwamba hawezi tena kupona.Mapema Agosti, Denaro mwenye umri wa miaka 61 alifanyiwa upasuaji wa utumbo katika hospitali ya San Salvatore mjini  L'Aquila. Lakini pamoja na upasuaji wake huko kufanikiwa hali yake ya kiafya iliendelea kuzorota kutoka na saratani kuongezeka.Denaro, mmoja wa watu wa karibu wa viongozi wakubwa wa zamani wa genge la Mafia, Bernardo Provenzano na Salvatore "Totò" Riina, anahusishwa na matukio mengi ya uovu. Aliwahi kuhukumiwa kifungo cha maisha pasipo kuwepo mahakamani.