1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHungary

Kiongozi wa Kanisa Katoliki awasili Hungary

28 Aprili 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili Hungary leo kuanza ziara ya siku tatu. Katika hotuba zake na mazungumzo na Waziri Mkuu Viktor Orban watajadili mambo mbalimbali.

Ungarn | Besuch Papst Franziskus in Budapest
Picha: Vincenzo Pinto/AFP/Getty Images

Francis atakutana na Orban hii leo na watajadili kuhusu vita vya Ukraine, uhamiaji na mizizi ya Ukristo barani Ulaya. Orban na Papa Francis wote wametoa wito wa amani na mazungumzo kuhusiana na vita nchini Ukraine, jambo ambalo Ukraine imeondoa uwezekano wa kufanyika.

Kwa ziara hii, Papa Francis anaitimiza ahadi yake ya kuizuru rasmi Hungary baada ya kupitia tu nchini humo kwa saa saba kufunga mkutano wa kanisa mjini Budapest mwaka 2021 alipokuwa njiani kuelekea Slovakia.

Hii ndiyo safari ya kwanza ya Francis tangu alipolazwa hospitalini kwa homa ya mapafu mnamo mwezi Machi. Siku ya Jumapili, Papa ataongoza misa nje ya majengo ya bunge mbele ya Mto Danube mjini Budapest.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW