1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV kuanza ziara barani Afrika wiki ijayo

9 Aprili 2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV anatarajiwa kuzitembelea nchi nne za Afrika kwa kipindi cha siku kumi kuanzia Jumatatu Aprili 13 hadi 23. Moja ya nchi atakayozitembelea ni Algeria.

Papa Leo XIV akiongoza misa mbele ya viwanja vya Mtakatifu Peter, Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIVPicha: Remo Casilli/REUTERS

Lengo la ziara hiyo ni kuwashawishi viongozi wa dunia kuyashughulikia masuala muhimu ya bara hilo ambapo kuna idadi kubwa ya Wakatoliki.

Mataifa atakayotembelea Papa Leo kwenye ziara hiyo ni Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta.  Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani atakuwa Papa wa Kwanza kuizuru Algeria, taifa lenye Waislamu wengi lenye takriban watu milioni 48 na Wakatoliki wasiozidi 10,000.

Mazungumzo na viongozi, wazawa yatazamiwa

Kwenye ziara hiyo itakayohusisha miji 11, atakutana na viongozi na kuzungumza na wazawa ambapo anatarajiwa kuhamasisha amani, majadiliano na kutoa ujumbe wa matumaini. Papa Leo XIV, anatazamiwa pia kutembelea maeneo ya kihistoria na yale yaliyoathiriwa na migogoro na majanga.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW