1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Papa Francis asema amani inawezekana

19 Novemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amerudia tena wito wa amani nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.

Papa Francis akionekana katika moja ya ibada, mjini Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amerudia kutoa wito wa amani Mashariki ya Kati na UkrainePicha: Gregorio Borgia/AP/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amerudia tena wito wa amani nchini Ukraine na Mashariki ya Kati wakati wa ibada ya leo Jumapili, akisema ilikuwa ni muhimu kuongeza jitihada za kuimaliza mizozo inayoendelea.

Amenukuliwa akiwaombea raia wanaoteseka nchini Ukraine na huko Israel na Palestina, mbele ya hadhara iliyokusanyika katika bustani ya Mtakatifu Petro.

Papa Francis amesema upo uwezekano wa kupatikana amani, lakini kunahitajika nia njema. Ameongeza kuwa jamii haitakiwi kukata tamaa kwa sababu kila wakati katika vita wanaonufaika na watengenezaji wa silaha pekee.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW