SiasaBurkina Faso
Traore: Uchaguzi "sio kipaumbele" Burkina Faso
30 Septemba 2023Matangazo
Traore ameeleza kuwa, hakutafanyika uchaguzi hadi nchi hiyo itakapokuwa salama na kumuwezesha kila mtu kupiga kura.
Traore ameyasema hayo katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa, karibu mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi.
Kiongozi huyo wa kijeshi, ambaye ameahidi kuirejesha Burkina Faso kwa utawala wa kidemokrasia na kufanya uchaguzi mnamo Julai mwaka 2024, pia ametangaza mabadiliko ya katiba ili kuwakilisha sura ya kitaifa.
Wakati Traore alipotwaa madaraka, alijipa "miezi miwili hadi mitatu" kuimarisha usalama, ila mwaka mmoja baadae nchi hiyo ya Afrika Magharibi bado inakabiliwa na mashambulizi kutoka makundi ya wanamgambo.