SiasaMadagascar
Kiongozi wa kijeshi Madagascar kuapishwa rasmi kuwa rais
15 Oktoba 2025
Matangazo
Hayo yameelezwa na vyanzo viwili vya kuaminika baada ya kufanyika mapinduzi ya kumuondoa madarakani rais Andry Rajoelina aliyeikimbia nchi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma kufuatia uhaba wa maji na kukatika kwa umeme.
Marekani imewatolea wito wadau wote nchini Madagascar kutafuta suluhisho la amani linaloheshimu katiba baada ya kikosi maalumu cha jeshi CAPSAT kutwaa madaraka.