Kiongozi wa Kundi la Patriotic Resistance Force,nchini Kongo afikishwa mahakama ya The Hague,Uholanzi
18 Oktoba 2007Matangazo
Germain Katanga kiongozi wa kundi la wapiganaji la Patriotic Resistance Force katika eneo la Ituri anakabiliwa na mashtaka sita ya uhalifu wa kivita na matatu ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika eneo hilo la mashariki ya Kongo. Katanga ni mshukiwa wa pili kufikishwa katika mahakama hiyo ya kimataifa baada Thomas Lubanga anayedaiwa kutekeleza uhalifu katika eneo hilo hilo la mashariki ya Kongo.
Thelma Mwadzaya alizungumza na Alexis Kanyenye mwanasheria na mwanaharakati wa kutetea haki za binaadamu katika eneo la Mashariki ya Kongo.Anaanza na kueleza namna hatua hiyo ilivyopokelewa.