1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Kiongozi wa RSF akutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Kiongozi wa kundi la waasi la RSF Mohamed Hamdan Daglo amesema jana kuwa alikutana na Rais w aUganda Yoweri Museveni, na kujadili naye matukio ya nchini Sudan, pamoja na maono yake juu ya majadiliano ya kukomesha vita.

Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Kiongozi wa kundi la waasi la RSF nchini Sudan Jenerali Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Hii ilikuwa mara ya kwanza ambapo Jenerali Mohamed Hamdan Daglo amethibitishwa kuonekana nje ya Sudan tangu kuzuka kwa vita kati ya kundi lake la RSF na jeshi la Sudan mnamo mwezi Aprili.

Rais Museveni alithibitisha mkutano huo kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, akisema alimkaribisha Daglo kwenye makazi yake ya shambani huko Rwakitura.

Kundi la RSF limekuwa likipata nguvu katika siku za karibuni na kufanikiwa kutwaa mji wa Wad Madani katikati mwa nchi.

Wapiganaji wake hata hivyo wameshtumiwa kufanya uporaji na kuua raia, madai ambayo linakanusha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW