Kiongozi wa magenge Haiti aapa kuendelea na mapambano
14 Machi 2024Matangazo
Cherizierambaye kwa jina la utani anaitwa "Barbecue" kupitia redio inayotangaza kwa lugha ya Kihispania ya W Radio, amesema muungano wake wa makundi yaliyojihami, haujali kuhusiana na kujiuzulu kwa Henry na kwamba wataendelea kupigania uhuru wa Haiti.
Cherizier ni afisa wa zamani wa polisi ambaye amewekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.
Mataifa yaanza kuwaondoa raia wao Haiti
Haiti haijafanya uchaguzi tangu mwaka 2016 na kwa sasa hakuna rais wala bunge. Hakukuchaguliwa mtu atakayemrithi rais Jovenel Moise ambaye aliuwawa mwaka 2021 huku Henry akiiongoza nchi hiyo baada ya kifo chake.