1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Kiongozi wa Malaysia ataka shinikizo kwa utawala wa Myanmar

10 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim ametaka nchi wanachama wenza katika umoja wa mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN zishinikize Myanmar kukomesha unyama dhidi ya raia wake.

Myanmar | Min Aung Hlaing
Picha: The Military True News Information Team via AP/picture alliance

Akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Thailand Anwar amesema ASEAN inapaswa kuwa na ari ya kutatua mgogoro wa Myanmar.

Baadhi ya wajuzi katika Umoja wa Mataifa wanauelezea mgogoro wa Myanmar kama vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababishwa na hatua ya jeshi kuchukuamadaraka kutoka serikali iliyochaguliwa kidemokrasia 2021 ya Aung San Suu Kyi.

Ameongeza kuwa ASEAN, inapaswa kutoa mapindekezo ya mbinu mpya ili kuakikisha vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya watu wa taifa hilo vinafikishwa mwisho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW