SiasaBangladesh
Kiongozi wa mpito wa Bangladesh atoa rai ya utulivu
7 Agosti 2024Matangazo
Pia amewarai waitumie fursa iliyopo ili kulijenga taifa bora. Amewasihi watu wote wajieupushe na vitendo vyovyote vya matumizi ya nguvu.
Yunus ametoa kauli hiyo siku moja kabla ya kurejea nchini Bangladesh kutoka Ulaya.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84 ataiongoza serikali ya mpito baada ya kufanyika maandamano yaliyomlazimisha Waziri Mkuu Hasina kuikimbia nchi. Yunus pia amesema ataitisha uchaguzi katika miezi michache ijayo.