1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNamibia

Kiongozi wa Namibia aliyepigania uhuru Sam Nujoma azikwa

1 Machi 2025

Maelfu ya wananchi wa Namibia pamoja na viongozi mbalimbali wamehudhuria Jumamosi hii hafla ya taifa ya kuuaga mwili na kumzika kiongozi wa nchi hiyo aliyepigania uhuru, Sam Nujoma.

Namibia Windhoek 2025 | Jeneza la Sam Nujoma
Jeneza la Sam Nujoma mjini Windhoek, NamibiaPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Nujoma, aliyeongoza kundi la wapiganaji wa SWAPO kutetea uhuru wa taifa hilo la kusini mwa Afrika,  alifariki Februari 9 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95. Rais wa sasa wa Namibia Nangolo Mbumba aliongoza mkusanyo huo na kumtaja Nujoma kama kiongozi mashuhuri ambaye urathi wake utakuwa nguzo ya kudumisha umoja.

Soma pia: Viongozi mbalimbali waomboleza kifo cha Sam Nujoma

Viongozi kadhaa wa Afrika akiwemo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Joao Lourenco wa Angola, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na maafisa wa kigeni kama spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo Hernandez wamehudhuria maziko yaliyofanyika muda mfupi baadaye na kupeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW