Kiongozi wa ngazi za juu ajiuzulu baada ya mashambulizi ya India
1 Desemba 2008Serikali ya India inashutumiwa kwa kutochukua hatua madhubuti za kijasusi huku ikitathmini uwezekano wa kusitisha mpango wa amani kati yake na nchi jirani ya Pakistan.
Mashambulio hayo yalitokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya yapata watu 172.Wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Deccan Mujahideen walishambulia eneo la kibishara la Mumbai pamoja na hoteli za kifahari za Taj Mahal na Oberoi.
Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama M K Narayanan naye pia amewasilisha waraka wake wa kujiuzulu japo haijabainika iwapo umekubaliwa.
Serikali ya India imeilaumu vikali nchi jirani ya Pakistan kwa kuhusika na shambulio hilo jambo inalokanusha.Katika ufunguzi wa mkutano wa pande mbili Waziri mkuu wa India Manmohan Singh alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usalama.
Nchi ya Pakistan kwa upande wake imekanusha madai ya kuhusika na mashambulio hayo na kuahidi kutoa ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.