1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas: Marekani inaweza kuizuia Israel isishambulie Rafah

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema Marekani ndio inaweza kuizuia Israel isiushambulie mji wa mpakani wa Rafah, na kuongeza kuwa kitakachotokea kitakuwa ni janga kubwa katika historia ya Wapalestina.

 Mahmud Abbas
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas Picha: Hamad I Mohammed/REUTERS

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema Marekani ndio inaweza kuizuia Israel isiushambulie mji wa mpakani wa Rafah, na kuongeza kuwa kitakachotokea kitakuwa ni janga kubwa katika historia ya Wapalestina. Abbas ametoa wito huo wakati wa mkutano wa kilele wa Jukwaa la Kimataifa la Uchumi duniani WEF, ulioanza mji mkuu wa Saudi Arabia wa Riyadh.

Kiongozi huyo wa Palestina amesema anaamini Israel itaishambulia Rafah ndani ya siku chache zijazo na kwamba shambulio lolote litawalazimisha Wapalestina kuukimbia Ukanda wa Gaza.

Israel ambayo imetishia kwa wiki kadhaa kuanzisha mashambulizi ndani na nje ya vitongoji vya mji huo kwa lengo la kuwaangamiza wapiganaji wa Hamas, imezidisha mashambuizi ya anga dhidi ya Rafah. Nchi washirika wa magharibi wa Israel ikiwemo Marekani zimetoa wito wa kujizuia kuushambulia mji huo unaopakana na Misri.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW