1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa UEFA atafakari kubakisha ligi ya mchezo mmoja

Sekione Kitojo
23 Agosti 2020

Rais wa shirikisho la kandanda Ulaya EUFA Aleksander Ceferin atafanya mazungumzo juu ya kuendelea na mfumo wa mtoano wa mkondo mmoja ambao umetumika kukamilisha msimu wa Champions League na Europa League.

UEFA Präsident Aleksander Ceferin
Picha: Imago Images/J. Huebner

 

Mfumo  huo  umetumika  kwa mintarafu ya kuokoa msimu huu  uliovurugika  kutokana  na  janga  la  virusi vya  corona  hata  hivyo  unaweza  kutumika  tu  katika  awamu  ya nusu  fainali.

Katika  mahojiano  na  shirika  la  habari  la  Associated Press siku ya  Jumapili, Ceferin  alisema  watu  ndani  ya   masuala  ya kandanda  na  nje  wamewasiliana  nae  na  kusema  walikuwa "wamefurahishwa mno" kutokana  na  mfumo wa  timu  nane katika fainali ambao  umeachana  na  mfumo  wa  michezo  miwili  ya nyumbani  na  ugenini katika robo  fainali  na  nusu  fainali.

Shabiki akipiga picha kombe la Champions League barani UlayaPicha: picture-alliance/NurPhoto/P. Fiuza

"Naweza  kusema  kuwa  mfumo  huu  wa  mchezo  wa  mkondo mmoja  unaonekana kuleta  hamasa  zaidi  kuliko  mfumo mwingine wa  michezo  miwili," Ceferin aliliambia shirika  la  habari  la AP kabla  ya  Paris Saint-Germain  kucheza  dhidi  ya  Bayern Munich katika  fainali  ya  Champions League.

Ceferin alisisitiza  kwamba  atashauriana  kwa  upana  kabla  ya kutafuta  mabadiliko  ya  kudumu  katika  mfumo.

Mfumo wa mtoano

"Ni moja  kati  ya  mambo yenye  kutia  msisimko ambayo yamesababishwa na  janga  hili," Ceferin alisema. "Tulilazimika kufanya  mfumo  kama  huu. Tulilazimika  kucheza  hivi, lakini mwishoni , tunaona  ni  mfumo  mzuri.

"Sasa , ni hali  tata  sana  kuweka  timu  nane  za  mwisho  katika kalenda.

Paris Saint-Germain na Bayern zinaoneshana kazi nani atanyanyua kombe la ubingwa wa Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa/F. Hoermann

Lakini  tuliona  kuwa watu wanataka msisimko katika  mchezo, ambao  katika  mchezo  mmoja , kila  timu inaweza  kuishinda nyingine katika  Champions League  ama  katika  Europa League. Kwa  hiyo  ni  kitu cha  kutafakari  hapo mbeleni ... Nafikiri  mwezi Septemba  ama  Oktoba, tunalazimika  kuanza  kuzungumzia  kwa dhati."

Ceferin hajali  kwamba  kuondoa  idadi ya michezo  ya  mtoano kunaweza  kuwa  na  athari  kubwa  kifedha katika  UEFA.

"Hata  kama  una  michezo  michache , thamani inaweza  kuwa  juu iwapo itafanyiwa matangazo  kwa  usahihi," alisema. "Naona marafiki zangu  katika  kandanda  na  nje  ya  kandanda  wakiwasiliana  nami na  kuniandikia  na  wote  wanaonesha  msisimko wa hali  ya  juu kwa  mfumo huu. Hakuna  mbinu  nyingi sana  uwanjani."

Makundi ya mashabiki

Kuzikusanya  timu nane mjini Lisbon  kukamilisha  Champions League  kunaonekana  kuliwezekana  tu  kwasababu  hakuna mashabiki walioruhusiwa  katika  viwanja  viwili kama  sehemu  ya vizuwizi vya  kusambaa  kwa  virusi  vya  corona, ikiwa  na  maana maafisa  wa  Ureno  hawakulazimika  kukabiliana  na  makundi  hasimu ya  mashabiki  ambao wangekusanyika  mitaani.

Mabingwa wa Europa League Sevilla ya UhispaniaPicha: Reuters/L. Baron

Mfumo  wa  timu  nne  za  mwisho  unawezekana  kuchukuliwa  katika mji  mmoja  katika  muda  wa  wiki  moja  na  kuleta  hamasa kama ya  mfumo  kama  wa  Super Bowl nchini  Marekani.

UEFA imekuwa tayari ikitafuta  njia  ya  kubadilisha  mfumo  wa Champions League  baada  ya  mwaka  2024.

Mfumo  wa  timu  nane  za  mwisho  tayari  iliwahi  kutumika kukamilisha  Europa  League na  Champions League  kwa  upande wa  wanawake mwezi huu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW