1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Kiongozi wa upinzani ahukumiwa kifungo cha miaka 2 India

23 Machi 2023

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini India Rahul Gandhi amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika kesi ya jinai ya kukashifu jina la ukoo la Waziri Mkuu Narendra Modi wakati wa uchaguzi mwaka 2019.

Indien - Kongresskundgebung gegen Inflation und Arbeitslosigkeit in Neu-Delhi
Picha: Kabir Jhangiani/ZUMA Press Wire/picture alliance

Gandhi, ambaye alihudhuria mwenyewe wakati wa hukumu mahakamani hapo, huko kwenye jimbo la nyumbani la Modi la Gujarat aliachiwa huru kwa kupewa dhamana.

Wakili wake amesema hukumu hiyo imezuiwa kutelezwa kwa siku 30 ili kumpa nafasi ya kukata rufaa. Katika mkutano wa hadhara wa 2019 katika jimbo la kusini la Karnataka, Gandhi aliuliza kwa kejeli kwa nini "wezi wote" wana jina la Modi."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW