1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kaliati ashtakiwa kwa kutaka kumuua Rais Chakwera

29 Oktoba 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi, Patricia Kaliati, amefikishwa mahamakami ambako anakabiliwa na tuhuma za kupanga kumuua rais wa nchi hiyo, Lazarus Chakwera.

Lazarus Chakwera
Rais wa Malawi Lazarus ChakweraPicha: AMOS GUMULIRA/AFP

Patricia Kaliati anakiongoza chama cha UTM cha marehemu Saulos Chilima aliyekuwa makamu wa rais wa Malawi aliyefariki kwenye ajali ya ndege mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Wakili wa mama huyo mwenye umri wa miaka 57 aliiambia mahakama kwamba mteja wake amechagua kunyamaza kimya akisubiri uamuzi wa mahakama kwa sababu anaamini kuwa hana makosa yoyote.

Katika kesi hiyo, Bi Kaliati anatuhumiwa pamoja na watu wengine wawili katika kupanga njama za kumuua Rais Chakwera. Watu hao ni Joseph Odala na Frank Chinedu ambao mpaka sasa hawajulikani waliko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW