Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Msumbiji Venancio Mondlane, amerejea nchini humo leo kutoka uhamishoni wakati vikosi vya usalama vikifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wake waliokusanyika karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa kumkaribisha kiongozi huyo nyumbani.