Kiongozi wa upinzani Msumbiji atangaza atarudi nchini
6 Januari 2025Mondlane, aliongoza maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi kwa zaidi ya miezi miwili akiwa nje ya nchi hiyo. Kiongozi huyo wa upinzani, aliondoka Msumbiji baada ya wakili wake kuuawa kwa kupigwa risasi mnamo Oktoba 19, anatarajiwa kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mavalane katika jiji la Maputo siku ya Alhamisi. Machafuko hayo yamesababisha hasara kubwa kwa uchumi wa Msumbiji, na yamesimamisha biashara ya mipakani. Usafirishaji wa meli, uchimbaji madini na shughuli za viwandani pia zimeathirika. Matokeo rasmi ya uchaguzi wa nchini Msumbiji yalionyesha kuwa Mondlane alipata asilimia 24 ya kura za urais huku mgombea wa Frelimo, Daniel Chapo aliibuka mshindi kwa kupata asilimia 65. Matokeo rasmi ya uchaguzi wa nchini Msumbiji yalionyesha kuwa Mondlane alipata asilimia 24 ya kura za urais huku mgombea wa Frelimo, Daniel Chapo aliibuka mshindi kwa kupata asilimia 65. Chama chake cha Frelimo kimetawala tangu Msumbiji ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni, Ureno mwaka 1975.