1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Machado awahamasisha wafuasi wa upinzani kupigania "ukweli"

17 Agosti 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, Maria Corina Machado awataka wafuasi wake "kuendelea na mapambano" wakati kukitarajiwa maandamano kote nchini Venezuela.

Maandamano ya Venezuela
Kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado pamoja na viongozi wengine wa upinzani wakiwasalimia wafuasi wao wakati wa kampeni za uchaguzi. Upinzani unapinga matokeo ya uchaguzi huo wa Julai 28Picha: JUAN BARRETO/AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, Maria Corina Machado jana Ijumaa aliwataka wafuasi wake "kuendelea na mapambano" wakati hii leo kukitarajiwa maandamano ya kupinga ushindi wa Rais Nicolas Maduro, ambao unakosolewa vikali ndani na nje ya nchi.

Machado ameitisha maandamano mapya katika miji zaidi ya 300 nchini Venezuela na nje ya nchi hii leo, ambayo ameyapa jina "Maandamano ya Kutetea Ukweli.

Yeye mwenyewe atashiriki maandamano hayo katika mji mkuu Caracas, ambako wafuasi wa chama tawala pia wamepanga kukusanyika.

Maandamano ya kumpinga Maduro yamesababisha vifo vya watu 25 hadi sasa na zaidi ya 2,400 kukamatwa tangu uchaguzi wa Julai 28 uliomrejesha madarakani kiongozi huyo.