Senegal: Mpinzani adai kunusurika jaribio la kuuawa
21 Machi 2023Sonko alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka katika kesi iliyochochewa kisiasa na ambayo ilisababisha machafuko makubwa wiki iliyopita.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook,jioni ya siku hiyo, Sonko alisema alipata matatizo ya kusikia maumivu ya tumbo,kizunguzungu na matatizo ya kushindwa kupumua.
Sonko ambaye ni mpinzani mkubwa wa rais Macky Sall amekuwa akitibiwa tangu alipodaiwa kushambuliwa kwa gesi ya kutowa machozi na kuumizwa wakati maafisa wa polisi walipomsindikiza kufika mahakamani alhamisi wiki iliyopita.
Soma pia: Ousmane Sonko atoa wito wa maandamano zaidi Senegal
Zaidi ya watu 400 wamekamatwa tangu wakati hup kwa mujibu wa mkuu wa mawasiliano wa chama cha Sonko,El Hadji Malick Ndiaye.Sonko amesema ataendelea kujiuguza nyumbani kuanzia hii leo baada ya polisi kuwahoji wahusika katika kliniki alikokuwa akipatiwa matibabu.