SiasaSenegal
Kiongozi wa upinzani Senegal atoa wito wa maandamano
15 Julai 2023Matangazo
Siku ya Alhamisi, gavana wa Dakar alitangaza kuwa mkutano huo uliopaswa kufanyika mchana wa leo umepigwa marufuku kutokana na hatari ya "kusababisha usumbufu kwa umma". Kutokana na zuio hilo, Sonko aliwaambia wafuasi wake kuwa, tarehe nyingine kwa ajili ya mkutano huo itatangazwa, lakini akaitisha maandamano Jumamosi jioni, yakikusudia kuonesha hali ya kutoridhishwa na kumtaka Rais Macky Sall aondoke madarakani kwa amani.
Alhamisi wiki hii, Sonko alipitishwa kwa kauli moja kwa njia ya kura na Chama chake kuwania nafasi hiyo. Ameteuliwa kugombea nafasi hiyo licha ya maswali juu ya kukidhi vigezo kutokana na rekodi yake ya kukutwa na hatia na vifungo jela.