1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa upinzani Tanzania ataka katiba mpya

12 Aprili 2021

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ametoa mwito kwa serikali mpya chini humo kulipa kipaumbele suala la katiba mpya na kufufua tena miito ya kutaka madaraka ya rais yapunguzwe.

Freeman Mbowe
Picha: DW/S. Khamis

Mbowe, mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani,Chadema kupitia hotuba yake hiyo iliyogusia hali ya taifa,alisema katiba ya sasa inampa mtu nafasi ya kuwa Dikteta au mfalme na kwahivyo serikali inapaswa kulipa kipaumbele suala la kuweka ratiba ya kufanyika mchakato wa kuibadili katiba.

Som pia: Uganda Tanzania zasaini mkataba wa bomba la mafuta

Kadhalika kiongozi huyo wa upinzani nchini Tanzania amemtolea mwito rais wa sasa Samia Suluhu Hassan kuharakisha pendekezo lake lililowasilishwa Jumanne wiki iliyopita la kuunda kamati ya kitaalamu ya wanasayansi ya kufanya utafiti juu ya ugonjwa wa Covid-19.

Mbowe ametoa wito wa kuwepo maridhiano kulirejesha taifa hilo katika kile alichokiita mkondo wa kidemokrasia.

Je hilo linawezekana? Zaidi Amina Abubakar amezungumza na Pasco Mayala mwaandishi habari na mchambuzi wa kisiasa nchini Tanzania.Sikiliza mahojiano. 

Freeman Mbowe atowa mwito katiba ibadilishwe Tanzania

This browser does not support the audio element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW