1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa upinzani Tanzania Freeman Mbowe ameachiliwa

23 Novemba 2024

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ameachiliwa kwa dhamana, chama chake kilisema leo,ikiwa ni baada ya kuzuiliwa zikiwa zimesalia chache kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tansania | Politiker der Opposition Freeman Mbowe wird verhaftet
Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe baada ya polisi kuzuia maandamano jijini Dar es salaam.Picha: Ericky Boniphace/DW

Uchaguzi huo unatazamwa kama kipimo cha Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua madaraka mwaka 2021 kwa ahadi za mageuzi na kuboreshwa kwa uhuru wa raia na kuwakatisha tamaa waangalizi wa kimataifa, ambao wanaashiria kurejea kwa sera za ukandamizaji za mtangulizi wake. Awali Ijumaa chama chake- CHADEMA kiliarifu kuwa yeye na watu wengine wa chama "wamezuiliwa kwa nguvu" na maafisa baada ya kutoka kwenye mkutano ambao polisi waliuvunja kwa kutumia vitoa machozi kusini mwa nchi hiyo. Ni mwezi uliopita tu, Mbowe na naibu wake Tundu Lissu pamoja na viongozi wengine wa upinzani waliwekwa kizuizini kwa muda mfupi baada ya polisi wa kutuliza ghasia kuzuia mkutano mkubwa katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam.