1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Kiongozi wa upinzani wa Msumbiji atangaza kurejea nyumbani

6 Januari 2025

Kiongozi wa upinzani wa Msumbiji ambayo ameongoza maandamano kwa zaidi ya miezi miwili sasa kupinga matokeo ya uchaguzi akiwa nje ya nchi, ametangaza kwamba atarejea nchini mwake kabla ya kuapishwa kwa rais mpya.

Msumbiji Venâncio Mondlane
Kiongozi wa upinzani wa Msumbiji, Venâncio Mondlane.Picha: Alfredo Zungia/AFP

Venancio Mondlane, aliyeondoka Msumbiji baada ya wakili wake kupigwa risasi na kuuawa mnamo Oktoba 19, ameandika kupitia mtandao wa Facebook kwamba atawasili uwanja wa ndege wa Mavalane siku ya Alkhamis.

Akiwa kwenye eneo lisilofahamika, mwanasiasa huyo ambaye anadai kushinda uchaguzi wa Oktoba 9, amewataka wafuasi wake kujitokeza kwa maandamano zaidi.

Soma zaidi: Baraza la katiba laidhinisha matokeo ya uchaguzi Msumbiji

Maandamano hayo yamekuwa yakikabiliwa na ukandamizaji wa polisi, na hadi sasa watu 300 wameshapoteza maisha, kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na mashirika ya haki za binaadamu.

Mondlane na wafuasi wake wanadai chama tawala cha FRELIMO, ambacho kimekuwapo madarakani kwa miongo mitano sasa, kiliiba uchaguzi wa Oktoba 9, baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza mgombea wake, Daniel Chapo, kushinda kwa asilimia 65, na kumpatia Mondlane asilimia 24.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW