Kiongozi wa upinzani wa Taiwan aitembelea China
7 Aprili 2026
Kiongozi wa upinzani wa Taiwan Cheng Li wun ameanza ziara ya kuitembelea China, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10. Kiongozi huyo wa chama cha Nationalist aliwasili leo Jumanne katika mji wa Shanghai akiandamana na ujumbe wake.
Ziara hiyo inafanyika katikati ya kiwingu cha kuongezeka mivutano kati ya Beijing na Taipei. Ziara ya mwisho kuwahi kufanywa na kiongozi wa chama hicho cha upinzani kinachoegemea upande wa Beijing, kinachofahamika pia kama Kuomintang au KMT ni mwaka 2016 wakati kikiongozwa na Hung Hsiu-chu.
China yaendelea na luteka yake ya kijeshi karibu na Taiwan
Kiongozi wa sasa,Cheng Li wun amesema anataraji ziara yake itatowa mwanga kwa jamii ya Kimataifa kuona fursa ya kutatua mivutano kwa njia za kidiplomasia na kuepusha vita.
Hata hivyo serikali ya Taiwan imemtahadharisha kiongozi huyo wa upinzani dhidi ya kujichukulia maamuzi.