Kiongozi wa waasi Nigeria, adai kutotenda kosa lolote
20 Januari 2022
Kiongozi wa kundi la wanaotaka kujitenga nchini Nigeria amekanusha kuwa na hatia ya mashtaka zaidi katika kesi yake ya ugaidi jana, miezi sita baada ya kukamatwa nje ya nchi na kurejeshwa nchini humo.
Matangazo
Nnamdi Kanu, kiongozi wa vuguvugu lililopigwa marufuku la Indegenous People of Biafra, IPOB ambalo linataka taifa tofauti la watu wa kabila la Igbo kusini-mashariki mwa Nigeria alikuwa tayari anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi na uhaini.
Lakini waendesha mashtaka katika mahakama ya Abuja waliongeza mashtaka mengine nane katika kesi yake ikiwemo uchochezi wa vurugu kabla ya kufikishwa kwake mahakamani hapo wiki hii, kulingana na timu yake ya mawakili.
Kanu amekana mashtaka hayo yote na mawakili wake wamewasilisha ombi la kufutwa kwa mashtaka yote, ambako kikao kingine cha kusikiliza hoja kimepangwa tarehe 16 Februari.
Tizama Picha:
Miaka 50 iliyopita: Mshikamano mkubwa Biafra
Vita vya Biafra mashariki mwa Nigeria vilitikisa jamii ya kimataifa miaka 50 iliyopita. Kimataifa walijaribu kusuluhisha miongoni mwao Wajerumani. Lakini wimbi hili la mshikamano limetoka wapi?
Picha: picture-alliance/Leemage/MP/Lazzero
Miaka 50 ya Biafra- paza sauti ya uhuru
Miaka miwili na nusu, maisha ya watu zaidi ya milioni mbili. Mnamo Januari 15,1970, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizika nchini Nigeria. Vita ambavyo vilitikisa umma pamoja na makali ya njaa. Nusu karne baadaye, hisia za Biafra kujitegemea zinazoongeneka. Wakati huo, Wajerumani wengi pia walizungumzia vita vya Biafra. Taswira ya nyuma baada ya miaka 50.
Picha: Getty Images/AFP
Vita kwa gharama ya wanyonge
Wajumbe wa Igbo ambao idadi kubwa ni Wakristo wa Nigeria, walikuwa wametangaza Jamhuri huru ya Biafra mnamo Mei 30, 1967. Karibu wakazi milioni 14 wa mkoa huo walisherehekea kuanzishwa kwake. Lakini mwaka mmoja baadaye vita vya kwanza vilitokea barani Afrika baada ya uhuru. Jina Biafra lilifanana na shida, njaa, kukata tamaa na vifo.
Picha: picture-alliance/Leemage/MP/Lazzero
Hasara kubwa
Wakati askari wa Nigeria walidhibiti mji wa bandari wa Harcourt mnamo Mei 1968, jimbo hilo lilipoteza njia yake ya kipee ya kuifikia baharini. Kuanzia wakati huo, watu walionaswa mjini humo walilazimika kutolewa kwa ndege - ushindi wazi kwa jeshi la Nigeria. Takriban wanamgambo 40,000 chini ya uongozi wa Jenerali Ojukwu walikuwa na vifaa na mafunzo duni ya kijeshi.
Picha: picture-alliance/United Archives/TopFoto
"Watoto wa Biafra"
Vikosi vya Nigeria vilianzisha vita vya kuwazingira wanamgambo na kuwaacha bila chakula. "Watoto wa Biafra" walijulikana kote ulimwenguni na harakati za mshikamano zilianza, janga la kibinadamu liliwaleta pamoja watu wote ulimwenguni. Idadi ya watoto na wazee waliokufa kwa njaa ilifikia hadi 10,000 kwa siku katika msimu wa joto wa 1968.
Picha: Gemeinfrei
Maandamano kwa watu wanaohitaji
Vita vya Biafra vilihamasisha watu nchini Ujerumani kuliko tukio jingine lolote Afrika. Mnamo Agosti 1968, wanafunzi wa Biafra na wa Ujerumani walianza matembezi ya siku tano kutoka Frankfurt kwenda Bonn. Wakishinikiza kutambuliwa kwa Biafra kama taifa la kidiplomasia na serikali huru. Bendera ya kitaifa ya Biafra ikiwa na jua linalochomoza.
Picha: picture-alliance/dpa/A. Hennig
Watu mashuhuri waliingilia
"Kama Wajerumani, tunapaswa kujua tunachosema tunapotamka mauaji ya kimbari ... kwa sababu kimya ni sawa na kutenda kosa hilo." Mwandishi Günter Grass alikuwa msemaji mashuhuri kwenye mkutano wa kupinga vita huko Biafra mnamo Oktoba 1968 mjini Hamburg. Mada hiyo iliwagusa wengi Ujerumani.
Picha: picture-alliance/AP Photo/ESH
"Njaa kwa ajili ya Haki"
Huko Ujerumani, maaskofu, wabunge na mashirika ya kijamii yalihusika - Siku ya maadhimisho ya kanisa la Kiinjilisti 1969 mada ilikuwa Biafra. Fedha na misaada zilikusanywa na kupelekwa maeneo yalioathirika Biafra. Rubani wa zamani wa Jeshi la Anga la Ujerumani Fryrich Herz, awali alipata mafunzo ya urubani wa kijeshi kutoka kwa jeshi la Nigeria alifikisha msaada huo kinyume na jeshi hilo.
Picha: picture-alliance/dpa/F. Reiss
"Kamati ya usaidizi" ikaundwa
Mjini Hamburg, wanafunzi Klaus Guerke na Tilman Zülch (pichani) waliunda "Kamati ya kuisaidia Biafra". Kamati hiyo ilipokea msaada kutoka kwa watu tofauti kama Meya wa Berlin, Heinrich Albertz, waandishi Günter Grass na Luise Rinser, na Askofu wa Münster, Heinrich Tenhumberg. Baadaye ikawa Jamii ya watu waliotishiwa.
Picha: picture-alliance/dpa/M. Schutt
Vita zaidi kwa mifumo ya mawazo
Mwanahistoria Golo Mann alisifu msaada uliolekezwa Biafra, jambo ambalo wakati huo halikueleweka na wanafunzi wenzake: "Vita ambavyo mabeberu wa Uingereza na wakomunisti wa Kirusi " walishindana kwa uhalifu, koloni la zamani ambalo lilidai kuweka umoja wa jimbo kwa kupigania kabila ambalo sio hata 'la kisoshalisti' ... nadharia yote ni hatari. "
Picha: picture-alliance/Keystone/Röhnert
"Biafra -Mamilioni wanakufa"
Huko London, waandamanaji waliandamana kutoka ubalozi wa zamani wa Jamhuri ya Kisovieti hadi katika ofisi ya waziri mkuu, mtaa wa Downing. Walipinga kwamba Umoja wa Kisovieti na Uingereza unaunga mkono vita vya Nigeria dhidi ya Biafra na usafirishaji wa silaha. Mwanasiasa wa chama cha wafanyakazi wa Uingereza Michael Barnes pia alizungumza katika mkutano ulioandaliwa na "Kamati ya Biafra".
Picha: Getty Images/Daily Express/R. Dumont
Ujumbe kwenye mabango
Wanaharakati wa kujitolea wa haki za binadamu walishangazwa na ukosefu wa ushirikino kimataifa. Matangazo kwenye magazeti, mabango yalikuwa na ujumbe mkali kudhihirisha mfadhaiko wao. Wajerumani maarufu kama Erich Kästner (pichani), Ernst Bloch, Paul Celan, Marcel Reich-Ranicki au Martin Walser walitoa uzito zaidi.
Picha: picture-alliance/akg-images
Misaada ya matibabu
Daktari wa Ufaransa Bernard Kouchner alisafiri kwenda Biafra mnamo 1968, ambapo, katika shughuli za shirika la msalaba mwekundu Kimataifa IRC, alijaribu kutoa misaada ya matibabu kwa watu wenye uhitaji. Kouchner alilaani msimamo wa IRK (Masomo ya dini ya Kiislamu) kutoingilia siasa za vyama vinavyopigana. Aliweka jiwe la msingi la asasi ya misaada ya "Madaktari Wasio na Mipaka".
Picha: Getty Images/AFP/D. Faget
Wito wa Biafra huru
Misaada kutoka kote ulimwenguni iliiweka Biafra hai. Makanisa na kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu yalitumwa mizigo 7,350 kwenye ndege ikiwa na uzito wa tani 81,300 za chakula na kudondoshwa kichakani. Biafra ililazimika kujisalimisha kwa serikali ya Nigeria mnamo Januari 15, 1970. Lakini wito wa Biafra huru bado unaendelea.
Picha: picture-alliance/Leemage/MP/Lazzero
Picha 131 | 13
Kanu alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015. Mwezi Juni mwaka jana, mwanasheria mkuu Abubakar Malami alitangaza kwamba Kanu allirejeshwa nchini Nigeria ili kukabiliwa na mashitaka yanayomkabili.
Maafisa hata hivyo hawakueleza mahali alipokamatwa Kanuna namna walivyomkamata. Lakini familia na wanasheria wake wamesema alikamatwa kinyemela nchini Kenya na kurejeshwa Nigeria.
Miito ya uhuru ama kujitenga huwa ni tete mno kusinimashariki mwa Nigeria, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa takriban miongo mitano iliyopita vilisababisha karibu watu milioni moja kufariki dunia kutokana na mapigano na hata njaa.