1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa waasi Syria akutana na rais Hollande

Admin.WagnerD24 Julai 2013

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Syria Jumatano hii anakutana na rais Francois Hollande, siku moja baada ya kuiomba Ufaransa itoe msaada wa kijeshi kuwaongezea nguvu waasi wanaopambana na utawala wa Assad.

HANDOUT - Ein undatiertes Foto zeigt Ahmed Assi al-Dscharba. Der von Saudi-Arabien unterstützte Stammesführer wurde in Isanbul zum neuen Vorsitzendend er syrischen opposition gewählt. Foto: SyrianNationalCouncil/dpa (ACHTUNG: Verwendung nur zu redaktionellen Zwecken bei vollständiger Quellenangabe "SyrianNationalCouncil" und unter Berücksichtigung der Creative Common Lizenz CC BY-SA 2.0 - beste verfügbare Qualität) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Ahmed Assi al-DscharbaPicha: cc by sa SyrianNationalCouncil / picture alliance / dpa

Kiongozi huyo mpya wa upinzani Ahmad Jarba, aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na wajumbe wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Ufaransa jana Jumanne, kuwa suala la kuomba msaada wa kijeshi ni moja ya malengo ya ziara yake ya siku mbili nchini Ufaransa.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande.Picha: Getty Images

Mkuu wa Jeshi Huru la Syria Jenerali Selim Idriss, aliongeza kuwa upinzani ulikuwa unafanyakazi na washirika wao wa Ulaya na Marekani ili kupata msaada wa kiufundi, afya na kibinaadamu, na kuongeza kuwa wanatumaini pia watapatiwa msaada wa silaha kwa kuwa waasi hawana zana za kutosha.

Hii ndiyo ziara ya kwanza ya Jarba nchini Ufaransa tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi wa muungano wa upinzani wa Syria SNC Julai 6, na alisema mwaliko wa rais Hollande ni ushahidi kuwa Ufaransa ina maslahi katika hatma ya Syria. Baada ya Ufaransa, Jarba ataelekea mjini New York Marekani kwa ajili ya mikutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Uingereza ilisema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 zikiwemo Urusi na China, litafanya mkutano wake wa kwanza na uongozi wa SNC siku ya Ijumaa.

Maafisa wa Ufaransa walisema mazungumzo na wapinzani yalikuwa yanapangwa kufanyika katika miji ya London na Berlin. Afisa wa juu wa Umoja wa mataifa alisema kuwa umoja huo umearifiwa kuhusu mashambulizi 13 yanayohusisha silaha za kemikali nchini Syria. Wataalamu wawili wa umoja huo walitarajiwa kuwasili mjini Damascus hii leo, kwa ajili ya mazungumzo na serikali.

Waasi wauteka mji muhimu wa Khan al-Assal

Lakini matumaini ya Umoja wa Mataifa kuchunguza matumizi ya silaha hizo yalipata pigo, baada ya waasi kuuteka mji muhimu wa Khan al-Assal kutoka kwa vikosi vya Assad siku mbili kabla ya kuwasili mjini Damascus kwa Ake Sellstrom, mkuu wa jopo la wachunguzi, na Angela Kane, ambae ni mkuu wa kitengo cha kupunguza nguvu za silaha cha Umoja wa Mataifa.

Kamanda mkuu wa Jeshi Huru la Syria FSA, Selim Idriss.Picha: John Thys/AFP/Getty Images

Mji wa Khan al-Assal ndiyo ulikuwa eneo la shambulizi baya la Machi 9, ambalo serikali ilisema lilifanywa na waasi ilipoutaka umoja wa mataifa kufanya uchunguzi. Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa, alisema itakuwa vigumu kwa wataalamu hao kuruhusiwa kuingia katika mji kama hauko katika udhibiti wa serikali.

Mataifa yote makubwa yanakubali kuwa silaha za kemikali zimetumiwa nchini Syria katika mgogoro uliyodumu miezi 28 sasa. Lakini mzozo kuhusu upande gani umetumia silaha hizo umekuwa chanzo kipya cha mgawiko juu ya Syria.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe
Mhariri: Saum Yusuf

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW